Friday, September 23, 2011

Rais Kikwete akutana na viongozi mbalimbali leo Rais Jakaya Kikwete akimkaribisha kwa mazungumzo Bwana Ted Alemayhu,Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa US Doctors for Africa aliyemtembelea Rais Kikwete katika hoteli ya Jumeirah iliyoko jijini New York.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na viongozi wa makampuni ya Sithe Global, iliyowakilishwa na Bwana Bruce Wrobel ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa makampuni hayo na Bwana Garrett Moran wa Blackstone Group  kuhusu uwekezaji katika Tanzania katika nyanja za Nishati na Miundombinu. Mazungumzo hayo yalifanyika katika hoteli ya Jumeirah huko New York.
 Rais Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Millenium Challenge Corporation Bwana Daniel Yohannes katika hoteli ya Jumeirah jijini New York mara tu baada ya Rais Kikwete kumaliza kuhutubia mkutano mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.PICHA NA JOHN LUKUWI.

Thursday, September 22, 2011

Rais Jakaya Kikwete akihutubia mkutano wa 66 wa Umoja wa Mataifa leo

Rais Jakaya Kikwete akihutubia mkutano wa 66 wa Umoja wa Mataifa jijini New York 

No comments: