Saturday, September 17, 2011

Rais Kikwete awaapisha wakuu wapya wa mikoa



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa walioteuliwa kushika nyadhfa hizo baada ya kuwaapisha katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo, asubuhi.

 Rais Dkt. Jakaya Kikwete , akimwapisha Mwantum Bakari Mahiza, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo asubuhi katika Viwanja vya Ikulu Dar. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha na kumkabidhi nyaraka za serikali, Joel Nkya Bendera, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Said Meck Sadik, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Magesa Stanslaus Mulongo, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amewaapisha wakuu wa mikoa aliowateua hivi karibuni.Sherehe za kuwaapisha wakuu hao wapya wa mikoa imefanyika leo asubuhi katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam.Pichani ni Mkuu mpya wa Mkoa wa Tabora. Bi.Fatuma Mwassa akila kiapo mbele ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete na kukabidhiwa miongozo ya kazi.

Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri mkuu, Mizengo Pinda, wakati wakiwa katika hafla hiyo ya kuapishwa wakuu wa mikoa leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mtoto Abubakar Mrisho Yasin, akiwa na Bi. Chiku Abdallah Sumbugallawa, aliyeapishwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantum Mahiza.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Abbas Hussein Kandoro, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Rais jakaya, akimwpisha, Christine Gabriel Ishengoma, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha, Saidi Thabiti Mwambungu, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Chiku Abdallah Sumbugallawa, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Leonidas Tutubert Gama, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Fabian Inyasi Massawe, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiteta jambo baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa Ikulu,jijini Dar es Salaam leo.

No comments: