Monday, September 19, 2011

Rais Kikwete awasili New York leo kuhudhuria mkutano wa 66 wa Umoja wa Mataifa



 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika hoteli ya Jumeirah Essex House jijini New York, Marekani, leo tayari kujiunga na viongozi wenzie wa dunia katika mkutano wa 66 wa Umoja wa Mataifa unaoanza kesho Jumatatu makao makuu ya Umoja wa Mataifa
 Rais Kikwete akipokewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe hotelini hapo. 

 Rais Kikwete akisalimiana na Afisa Habari katika ubalozi wa Tanzania Umnoja wa Mataifa, New York Bi Maura Mwingira
 Rais Kikwete akisalimiana na Bw. Mero wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
Rais Kikwete akisalimiana na Dkt Kaushik Ramaiya wa Hospitali ya Hindu Mandal, Dar es salaam
 Baadhi ya maafisa wakiwa katika chumba cha mkutano wa maandalizi
 Dkt Rachel Mhaville na Dkt Linda Ezekiel wote toka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika mkutano huo wa maandalizi
Kaimu Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali Bw. Mkumbwa Ally (kati) akiwa na maofisa wengine
Rais Kikwete akisalimiana na Profesa Kulikoyela Kahigi, Mbunge wa Bukombe (CHADEMA) huku Mbunge wa Liwale Mh Fath Mitambo na Katibu Mkuu Wizara ya afya Mama Blandina Nyoni wakisubiri
Rais Kikwete akisalimiana na Mwambata wa Jeshi katika Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Kanali  Wilbert Ibuge
Rais Kikwete akisalimiana na Dkt Rachel Mhaville ambaye ni daktari bingwa wa meno ya watoto kutoka hospitali ya taifa ya Muhimbili ambaye anahudhuria mkutano huo pamoja na maafisa waandamizi wizara ya Afya
Rais Kikwete akipeana mikono na Bw. Omar Mwalimu ambaye ni msaidizi wa Waziri wa Afya wa Zanzibar
Rais Kikwete akisalimiana na maafisa 
Maafisa mbalimbali kutoka Tanzania na wa ubalozi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa wakiwa kikaoni
Rais Kikwete akiongoza kikao cha maandalizi kwa ajili ya mkutano huo wa kila mwaka wa  Umoja wa Mataifa

No comments: