Saturday, September 17, 2011

Rais Jakaya Kikwete ashiriki katika swala ya pamoja kuombea marehemu wa ajali ya meli Zanzibar, mabalozi wamiminika kutoa pole




katibu mkuu kiongozi Philemon Luhanjo akitoa tamko la serikali kuhusiana na ajali ya meli ya Spice Islander iliyotokea mwishoni mwa wiki.
 Swala ya kuombea marehemu
 Kinamama wakishiriki katika swala hiyo
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(watatu kutoka kushoto) akijumuika na  baadhi ya viongozi wa Serikali  na wananchi wa Zanzibar katika dua ya pamoja ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali ya meli iliyotokea mwishoni mwa wiki eneo la Nungwi,Unguja.Viongozi wengine katika picha kutoka kushoto ni Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Seif Shariff Hamad,kushoto kwa Rais Kikwete ni Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohammed Gharib Bilal,Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali  Iddi  na Rais Mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi.
Baadhi ya wananchi wa Zanzibar wakiswali wkati wa dua maalumu ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali ya meli ya Spice Islander iliyotokea mwishoni mwa wiki eneo la Nungwi,Unguja.Swala hiyo ya pamoja ilifanyika leo(sept 12) katika viwanja vya Maisara.



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwafariji na kuwapongeza wananchi wa kijiji cha Nungwi kufuatia juhudi zao za kujitolea kuwaokoa watu waliopata ajali katika meli ya MV.Spice Islanders iliyotokea juzi usiku.Meli hiyo ilikuwa ikitokea Unguja kwenda Pemba amapo watu zaidi ya 200 wanahofiwa kufa maji.Abiria 602 wameokolewa wakiwa hai.
Balozi wa Marekani nchi Tanzania Alfonso Leinhardt akimfariji Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia ajali ya meli ya Spice Islanders iliyotokea huko Nungwi, Unguja juzi usiku ambapo watu zaidi 200 wamepoteza maisha na wengine 602 kuokolewa wakiwa hai.Picha na Freddy Maro



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Kufuatia msiba mkubwa uliotokana na ajali ya kuzama kwa meli ya Spice Islander katika bahari ya Hindi usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, Septemba 10, 2011, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, ameamuru maombolezo ya kitaifa kwa muda wa siku tatu kuanzia kesho tarehe 11 Septemba, 2011 ambapo bendera nchini zitapepea nusu mlingoti.

Aidha, kufuatia msiba huo, Mheshimiwa Rais, ameahirisha ziara rasmi ya kiserikali ya siku tatu nchini Canada ambako alikuwa amealikwa na Gavana Mkuu wa nchi hiyo, Mheshimiwa David Johnston. 

Katika ziara hiyo iliyokuwa ifanyike kuanzia tarehe 14 – 16 Septemba, 2011, Mheshimiwa Rais angekutana pia na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mheshimiwa Stephen Harper.  Mheshimiwa Rais ameiomba Serikali ya Canada kupanga ziara hiyo kwa tarehe za baadaye.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.



 Balozi wa Khazkstan nchini Abu Dhabi,akiwesa saini katika kitabu ya Maombolezo kwenye ubalozi wa Tanzania nchini humo.
Balozi wa Khazkstan nchini Abu Dhabi akipeana mkono wa pole na Balozi wetu nchini humo,Mh. Mohamed Maharage.
Balozi wetu nchini Abu Dhabi ,Mh. Mohamed Maharage akikumbatiana na Balozi wa Bernin nchini humo mara baara ya kupokea rambi rambi toka kwa jumuiya ya mabalozi nchini humo.
Balozi wa Philipines nchini Abu Dhabi akitia saini katika kitabu cha maombolezo kwenye ubalozi wetu nchini huko.
Balozi wa Ukraine akipeana mkono na Balozi Maharage.
Balozi wa Poland akitoa rambi rambi zake kwa Balozi Maharage.
Balozi wa  Belarus
Balozi wa Egypt nae alifika katika ubalozi wetu nchini Abu Dhabi kutoa rambi rambi zake.

No comments: