Saturday, September 17, 2011

SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA NAIBU KATIBU MKUU UMOJA WA MATAIFA



 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro akisaini kitambu cha maombolezo kilichofunguliwa  katika Ubalozi wa  Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, kufuatia ajali ya kuzama kwa meli  MV Spice Islander.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro akipeana mkono wa pole  na Mhe. Ombeni Sefue, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro amewatumia  salamu za pole Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na  Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya MV Spice Islander iliyotokea  tarehe 10 Septemba 2011.

Katika salamu zake kwa viongozi hao pamoja na watanzania wote, Dkt. Migiro anasema  ameshtushwa na kusikitishwa sana na taarifa za ajali hiyo. Hata hivyo ameguswa na kupata  faraja kubwa  mno, kwa namna ambavyo serikali hizo mbili, na kwa kushirikiana  na wananchi  wake zilivyoweza kuratibu  na kusimamia  zoezi  zima la ukoaji wa  abiria walionusurika  na  uopoaji wa miili ya  marehemu.

Naibu Katibu Mkuu  anasema,kama alivyosema Katibu Mkuu  Ban ki Moon katika salamu zake kwamba, Umoja wa Mataifa upo pamoja na watanzania katika kipindi hiki  kigumu. Aidha Dkt, Asha-Rose Migoro anasema   dua na sala zake anazielekeza kwa waathirika na familia zao, na anawatakia nafuu ya haraka  majeruhi wote.

IMETOLEWA NA UBALOZI WA TANZANIA  UMOJA WA MATAIFA

No comments: